Wakulima wanaweza kuuza moja kwa moja kwenye jukwaa la Selina Wamucii kama vikundi vilivyosajiliwa, na kujiunga pamoja. Wakulima wanadhibiti mchakato mzima kuanzia kwenye ulimaji, uvunaji na usambazaji moja kwa moja katika masoko ya ndani ya nchi zao, barani Afrika au hata kuuza popote pale ulimwenguni wao wenyewe.

Mahitaji:

  1. Unahitaji kuwa mwanachama wa kikundi cha wakulima
  2. Kikundi kinahitaji kusajiliwa rasmi chini ya sheria za nchi yako.
  3. Inaweza kuwa kikundi cha aina yoyote, kama vile kikundi cha kusaidiana, shirika la jamii, nk.
  4. Kuwa na cheti rasmi cha usajili kwa kikundi hicho.
  5. Kikundi kinahitajika kuwa na wanachama hai wasiopungua 50.
  6. Kikundi kinapaswa kuwa na muundo unaoeleweka wa uongozi.
  7. Kikundi kiwe kimehifadhi vema kumbukumbu za muhtasari wa mikutano.
  8. Wanachama wote wa kikundi wanatakiwa wawe wanalima angalau aina moja ya zao kuu.
  9. Kwa kuanzia, Selina Wamucii itatoa kipaumbele cha utafutaji masoko kwa zao kuu pekee.
  10. Unaweza kuorodhesha bidhaa nyingi zaidi, lakini kila bidhaa unayoongeza lazima iwe inazalishwa na idadi kubwa (zaidi ya nusu) ya wana kikundi.

Ikiwa hautatimiza mahitaji haya, tunakutia moyo kuhamasisha wakulima wenye nia moja katika eneo lako, kujiandikisha kikundi, kukidhi mahitaji kisha kujiandikisha.

Ikiwa unatimiza mahitaji tuliyoorodhesha hapo juu, tafadhali sajili kikundi chako hapa chini.